Singida
JESHI la Polisi mkoani Singida linamtafuta kijana mmoja mkazi wa Kibaoni katika
manispaa hiyo kwa tuhuma za kumlawiti
mwenzake na kumharibu vibaya sehemu za haja
kubwa baada ya kumnunulia pombe kali aina
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Geofrey
Kamwela, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi
saa 3:00 usiku eneo la soko la Kibaoni, kata ya
Kindai, na kumtaja mtuhumiwa huyo kwa jina
Alisema kuwa baada ya kila mmoja kumaliza
kunywa viroba vyake, kijana aliyelawitiwa (jina
tunalihifadhi) alimweleza mtuhumiwa kuwa
amelewa kupindukia na hivyo kila mmoja
arejee nyumbani kwao.
“Walipofika eneo la soko la Kindai, muathirika
alimwambia mtuhumiwa amwache hapo ili
apumzike kwa vile pombe ilikuwa imemzidi
sana lakini ghafla alianguka chini na kisha na
kupoteza fahamu,” alisema.
Baada ya muathirika kupoteza fahamu,
mtuhumiwa alitumia fursa hiyo na kuanza
kumwingilia kimwili kinyume cha maumbile.
Alisema kuwa wasamaria wema walimshuhudia
mtuhumiwa akiendelea kufanya unyama huo
dhidi ya rafiki yake lakini walipojaribu
kumkamata, aliwaponyoka na kukimbilia
kusikojulikana.
“Raia wema hao walimbeba muathirika na
kumpeleka nyumbani kwake na baadaye aliweza
kupata fahamu ndipo alianza kusikia maumivu
makali sehemu yake ya haja kubwa,” alisema.
Alisema muathirika alipelekwa hospitali ya
mkoa wa Singida ambako alibainika kuharibiwa
vibaya sehemu zake za haja kubwa.