
ZAMANI kulikuwa na kasumba kwamba wanaume ndiyo huwapiga wanawake lakini hivi karibuni kibao kimegeuka ambapo mama mjasiriamali, aliyetajwa kwa jina moja la Mama Ashura ambaye ni mfanyabiashara wa viazi mviringo, anadaiwa kuwapa kipondo njemba watano kisa deni.
Baada ya zogo kuwa kubwa huku umati ukifurika eneo hilo, mmoja wa mashuhuda hao alimtonya mwanahabari wetu ambaye alifika fasta na kushuhudia mama huyo akipambana vilivyo na kundi la wanaume hao ambao aliwashinda nguvu kwa kuwashushia ngumi za kutosha. SOMA ZAIDI>>>>