Quantcast
Channel: MAMBO YA WALIMWENGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2863

MSANII HUYU WA BONGO MOVIE AAMINI NDOA NI CHUO CHA MAFUNZO BAADA YA KUOLEWA.

$
0
0
 
Halima Yahya ‘Davina’.

MSANII wa filamu za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ amekiri kujifunza mambo mengi ya maisha baada ya kuingia kwenye ndoa.Akizungumza na mwandishi wetu, Davina alisema kwamba anaichukulia ndoa yake kama chuo cha mafunzo kwa jinsi alivyobadilika na kuwa tofauti na Davina aliyekuwa nje ya ndoa.
“Nimekuwa tofauti kabisa na Davina wa kabla ya ndoa, sasa hivi kila kitu nakifanya kwa ustaarabu kwa kuwa najiona nimekuwa mwenye majukumu mengi,” alisema.
Akifafanua zaidi, Davina alisema zamani alikuwa ni mtu wa kurandaranda hovyo tofauti kabisa na hivi sasa.

“Zamani nilikuwa napenda safari zisizokuwa na faida tofauti na sasa hivi, kweli nimeamini ndoa ni chuo cha mafunzo,” alisema huku akiwaombea wasanii wenzake walio nje ya ndoa wafunge ndoa na kuwa na familia zao kwani watajifunza mengi. 
-GPL

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2863

Trending Articles