Mnenguaji wa bendi ya African Stars Mandela juzi usiku alitoa mpya ya mwaka baada ya kulazimisha penzi kutoka kwa dada nnoja aliyefahamika kwa jina moja la ZainabTukio hilo lilitokea nje ya ukumbi wa Mango Garden ambako bendi ya Afican Stars ilikuwa ikifanya onyesho la sikukuu ya Krismas.
Mara baada ya bendi hiyo kumaliza kufanya onyesho hilo majira ya saa tisa na nusu mnenguaji huyo alienda katika baa ya Uhuru Pic ambapo alimwita msichana huyo ili waondoke lakini kulitokea kama mtafaruku kwani msichana huyo alikataa katakata kuondoka na mnenguaji huyo.
Baada ya kuona hivyo mnenguaji huyo ili mbidi atumie nguvu kumvutia ndani ya bajaji dada huyo ambayo haikuwa kazi laisi ndipo mtafakuru ukazuka.
Hata hivyo dada huyo baada ya kupata upenyo alichurupuka na kutoka mbio na kudandia bajaji ingine na kuondoka kwa kasi.