Quantcast
Channel: MAMBO YA WALIMWENGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2863

WASTARA-- SITAKI KUCHUNGUZWA

$
0
0

MWIGIZAJI, Wastara, aliyekuwa mke wa Sajuki (marehemu sasa), amewajia juu wale wote wanaomchafua jina kwa kuwaambia kuwa wasitafute fedha kwa kumzushia kashfa.  
Kauli yake imekuja baada ya kuanza kuandikwa kwa mtazamo tofauti akisema yeye ni miongoni mwa waigizaji wasiokuwa na kashfa.

Alisema kuwa hataki kuingia kwenye mizozo na watu, hivyo ni bora wakamwacha aendelee kujipanga upya katika maisha yake.

“Sipendi kushushiwa heshima na wala kuingia kwenye migogoro na watu ambao wengine nimekuwa nao, waniheshimu na wasiniandike vibaya,” alisema Wastara.
Wastara aliongeza kuwa haijalishi ana uhusiano wa kimapenzi na nani, lakini kama binadamu anahitaji kuwa na maisha binafsi.

“Kuna baadhi ya watu hawawezi kukaa na kufanya shughuli nyingine zaidi ya kutafuta fedha kwa nguvu kwa kutumia majina ya watu wengine, naomba waniache nifanye mambo yangu na kuendesha maisha yangu, wakija kikazi tufanye kazi, lakini kama ni majungu na kunichunguza sitaki,” alisisitiza.
Credit: Mwanasporti

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2863

Trending Articles