Umeshawahi kujikuta umekutana na msichana mrembo au mvulana mtanashati, halafu siku ya pili ukakutana na pacha wake wanaofanana hadi ukucha na ukaendeleza maongezi mlipoishia jana bila kugundua si yule wa jana? Basi ndicho kilichomtokea Diamond Platnumz.Coke Studio walimuandalia Platnumz ‘blind date’ ya mtoto wa kike mrembo, ila bila yeye kujua kuwa wako wawili mapacha wanaofanana (identical twins) na kumchezea mchezo. Baada ya kukutana na msichana wa kwanza anayeitwa Rose, walizungumza kwa muda mfupi kisha mtoto huyo wa Kikenya akaomba kwenda washroom. Huko alikuwa anasubiri pacha mwenzie aitwaye Janet ambaye walibadilishana, aliyerudi kwa Diamond hakuwa yule wa mwanzo.
Ila mwisho wa mchezo meneja wa Diamond alijifanya kumuita pembeni kumuelekeza jambo, ndipo hapo walipojitokeza mapacha wote wawili na kuketi pale pale alipokuwa Diamond, aliporudi akapigwa na butwaa asijue ni yupi aliyeanza kuongea naye maana hata nguo walizovaa zinafanana.
Tazama video ufahamu ‘blind date’ iliishaje