Mtoto Bernard Benjamin enzi za uhai wake.
MTOTO wa miaka sita, Bernard Benjamin ambaye alikuwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Nyamunge, wilayani Ilemela jijini Mwanza, amesombwa na mafuriko na mwili wake kukaa siku kumi na tano bila kuharibika.
Tukio hilo lilijiri Desemba 2, mwaka huu kwenye Mto Kenge jijini hapa, maeneo ya Mabatini, Wilaya ya Nyamagana baada ya kujaa maji ambapo marehemu alisombwa na mafuriko hadi pembezoni mwa Ziwa Victoria.
Baba mzazi wa marehemu Bernard, Benjamin David alisema siku ya tukio yeye alikuwa safari na mama wa mtoto alikuwa kazini, watoto walibaki na msichana wa kazi nyumbani.
“Ilikuwa Jumanne asubuhi, mvua kubwa sana ilinyesha kwa saa moja na nusu hivi na kusababisha mafuriko. Watoto wangu wote walikuwa nyumbani, lakini mvua ilipokatika walitoka nje na kuanza kucheza.SOMA ZAIDI>>>