Mama Salma kikwete
MAMA SALMA ;
Swali: Ni ipi historia fupi ya maisha yako?
Jibu: Mimi naitwa Salma Rashid. Nilizaliwa katika wilaya ya Lindi Mjini, Novemba 30, 1963. Baba yangu anaitwa Rashid Yussuf Mkwachu na mama yangu ni Mwanapaza binti Shariff.
Kwa asili, baba yangu anatoka Sarai, Rufiji mkoani Pwani na mama yangu anatoka Lindi.
Katika familia yetu, upande wa mama, tulizaliwa watoto saba, wasichana watatu na wavulana wanne. Mimi ni wa sita, ila kwa baba ni wa pili, nina kaka yangu na mdogo wangu. Nina wadogo zangu wengine watatu ambao tunachangia baba, kati yao wavulana ni wawili na msichana mmoja.
Baba yangu alikuwa mfanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyovunjika mwaka 1977 na kituo chake cha kazi kilikuwa Mtwara, wakati baba anafanya kazi, mama alibaki Lindi, hali ambayo ilinifanya nipate elimu yangu ya msingi kuanzia mwaka 1973 katika shule nne tofauti; Nnaida ya Mikindani, Mtwara, Rahaleo ya Lindi, Ligula (Mtwara) na Stadium, Lindi ambapo nilimalizia elimu yangu ya msingi.SOMA ZAIDI>>