Quantcast
Channel: MAMBO YA WALIMWENGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2863

MTOTO WA KITANGA CHUCHU HANS AJIGAMBA KUWA RAY HAPINDUI KWAKE!

$
0
0
 
Staa wa sinema za Kibongo, Chuchu Hans (katikati) akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar.

Mahaba mahabani! Staa wa sinema za Kibongo, Chuchu Hans amefunguka kuwa staa mwenzake ambaye ni mwandani wake, Vincent Kigosi ‘Ray’ amefika kwenye penzi lake ndiyo maana ametulia kwani amepata ‘malovee’ aliyokuwa akiyatafuta siku zote.Chuchu alitoa kauli hiyo kwenye sherehe fupi ya kuzaliwa kwake iliyofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar ambapo alikwenda kujumuika na watoto wachanga hasa wale waliofiwa na wazazi wao pamoja na waliozaliwa siku hazijatimia ‘premature’

 
Chuchu Hans akiwa na Ray.
 Staa huyo alisema hivi sasa Ray hafurukuti kwake kwani anampa mapenzi motomoto. “Hapa Ray amefika aambiwi kitu,” alisema Chuchu.Alipoulizwa sababu ya kusherehekea hospitalini hapo aliweka wazi kuwa ilitokana na yeye kuzaliwa ‘premature’ na mwanaye kumzaa akiwa ni premature hivyo aliona awakumbuke watoto wa aina hiyo na waliozaliwa na kufiwa na wazazi wao huku wakiwa wodini.

Chuchu aliyeongozana na wasanii kadhaa, aliwapatia watoto hao zawadi mbalimbali.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2863

Trending Articles