Na Deogratius Mongela
KW/RB/8441/2014 imemshikilia Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga kwa madai ya kuzichapa na Miss Tanga 1997, Mona Faraja ambaye pia ni mke wake na kumsababishia majeraha, Risasi Jumamosi lina ‘full’ stori.

Ishu hiyo iliyonyakwa laivu na majirani ilijiri usiku wa Jumatano iliyopita maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar, nyumbani kwa Lundenga wakati wawili hao walipokuwa wamepumzika baada ya mihangaiko ya mchana kutwa.Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, wakiwa wanabadilishana mawazo, mara simu ya Lundenga iliita na ndiyo chanzo cha mtafaruku, upi huo?
TUJINGE NA CHANZO
Mtoa habari wetu alisema kuwa, tatizo lilikolea mara baada ya simu hiyo kuita mfululizo kwa namba ngeni iliyodaiwa kuwa ni ya ‘kichenchede’ cha pembeni huku bosi huyo akiwa hana mpango wa kuipokea.SOMAZAIDI>>