Maswahiba: Rais wa Real Madrid, Florentino Perez ameitete sera ya usajili ya kalbu hiyo baada ya maoni ya Cristiano Ronaldo
RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez ameitetea sera ya klabu yake ya usajili baada ya Cristiano Ronaldo kufunguka ya moyoni akipinga kuuzwa kwa Angel di Maria katika klabu ya Manchester United kwa dau la paundi milioni 60.
Mabingwa hao wa Ulaya pia walimuuza kiungo wa kimataifa wa Hispania Xabi Alonso katika klabu ya Bayern Munich kwa dau la paundi milioni 5, kitu ambacho kimemvunja moyo Ronaldo ambaye aliponda waziwazi maamuzi ya Perez.
Wametengana: Ronaldo na Angel di Maria walionesha ushirikiano mkubwa Bernabeu kabla ya mmoja kuondoka

Dili lilikamilika: Mabingwa wa Ulaya, Real Madrid walimuuza Di Maria kwa Mancester United na kuvunja rekodi ya usajili nchini England.
"Nimesikiliza maoni aliyosema Ronaldo na kama ninavyomjua, kamwe haiulizi klabu. Uhusiano wangu na yeye uko kamili, hakuna tatizo lolote. Cristiano ndiye mchezaji bora wa dunia, hilo liko wazi"
Perez aliweka wazi kuwa Real Madrid haikuwa na jinsi zaidi ya kumuuza Di Maria kufuatia kugoma kuongeza mkataba ambao ungemfanya awe mchezaji wa pili kwa kulipwa vizuri katika klabu.
"Nimekuwepo hapa tangu mwaka 2000", Perez aliendelea."Tangu hapo wachezaji wengi wamekuja na kuondoka na uzoefu wangu unaniambia kwamba wachezaji wengi wanaoondoka wanakuwa bora zaidi na wanaokuja wanazua maswali"
"Usajili wangu wa kwanza ulikuwa (Zinedine) Zidane na wa mwisho (kabla ya dirisha la majira ya kiangazi) alikuwa (Gareth) Bale. Na tulitoa ofa nzuri kwa Di Maria na alikataa".