Kanisa hilo lililopo maeneo ya Kawe jijini Dar limetoa shukrani zake za dhati kwa Mwenyezi Mungu kuwawezesha kumiliki helikopta hiyo ambayo itatumika zaidi kutoa huduma sehemu mbalimbali za Tanzania na duniani kote.
Helkopta hiyo inakadiriwa kugharimu shilingi bilioni 7.5.
Misa hiyo iliyoanza majira ya asubuhi mpaka jioni ilifanyika kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers ambapo ilihudhuriwa na waimba injili maarufu nchini wakiwemo; Rose Mhando, Upendo Nkone, Christina Shusho, Flora Mbasha, John Lissu, Boniface Mwaitege, Munishi na wengineo.
Picha/Stori na Gabriel Ng’osha na Shani Ramadhani/GPL