

Kwenye msg yenyewe, Gail aliandika kumshukuru mpenzi wake kwamba aliinjoy walipotoka pamoja usiku mmoja, na kumwambia ‘natamani tungekua tunafanya hivi mara kwa mara’.
Taarifa imesema Askari huyu ambae ni mama wa watoto wawili alikua akishiriki kwenye penzi la nje na askari mwenzake wakati mumewe akiwa kwenye safari za kibiashara ambapo baada ya kukosea msg aliamua kujiua kwa kunywa vidonge vingi na kujilaza kwenye buti ya gari.
Hata hivyo pamoja na Mwanamke huyo kutoka nje ya ndoa, mume wake ambae wamekua kwenye ndoa kwa miaka 30, Peter Crocker mwenye miaka 49, amesema Gail alikua Mwanamke wake wa maisha.