MAMA mzazi wa marehemu Hussein Mkiety ‘Sharo Millionea’, Bi. Zuwena Mkieti amewataka waandaaji wa filamu za Kitanzania kusitisha mara moja matumizi ya sinema za mwanaye huku akishusha lawama nzito.
Mama Sharo.
Akizungumza kwa njia ya simu na ‘kiranja’ wetu mwanzoni mwa wiki hii, mama huyo alidai kujisikia uchungu kuona kazi za mwanaye zinazidi kuingia sokoni huku familia yake ikiambulia patupu.“Ninasikitika sana kuona kuna muvi ambazo zinatoka ndani yake amecheza Sharo, sina taarifa yoyote hivyo naomba wasitishe mara moja au vinginevyo waje kwangu tuzungumze kabla ya kuingiza kazi za mwanangu sokoni ili nami nipate angalau chochote,” alisema Mama Sharo