WADAU KUMRADHI KWA PICHA IFUATAYO HAPO CHINI KAMA ITAWAKWAZA.
. (Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Mtoto mchanga amezaliwa katika hospitali ya mkoa wa Singida akiwa hana baadhi ya sehemu za mwili kuanzia kifuani hadi kichwani.
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida Dkt. Joseph Malunda, amesema hospitali ya mkoa wa Singida ni mara ya kwanza kuzaliwa kiumbe kama hicho tangu kuwa hospital ya mkoa.
Dkt. Malunda amesema watoto hao ambao wamezaliwa mapacha wote wa kike wakiwa na miezi saba, mmoja ambaye ana viungo vyote alikuwa na kilo 1.3 lakini alifariki baada ya saa sita kupita.
Dkt. Malunda amesema baada ya mama mzazi wa watoto hao Amina Bilau kujifungua mtoto wa kwanza, waliona mtoto mwingine akifuatia na ndipo alipojifungua kitoto hicho chenye kilo 1.4 ambacho hakina mikono ,kifua,na kichwa
Kutokana na hali hiyo Dkt. Malunda amewashauri wakina mama wanapopata uja uzito kuhudhuria kliniki na kuacha kutumia madawa makali pindi wanapokuwa wajawazito.
Dk. Malunda amesema madawa ya aina hiyo yanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kuzaliwa watoto ambao wanakuwa na mapungufu ya viungo.
Akieleza huku akiwa amelazwa katika hospita ya mkoa wa Singida mama huyo Amina Bilau ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mtamaa kata ya Mwankoko Manispaa ya Singida, amesema yeye aliona tumbo lina kuwa kubwa na baada ya kupata matibabu katika zahanati ya kijiji bila mafanikio aliamua kwenda katika hospita ya mkoa wa Singida na kijifungua watoto akiwa katika hali hiyo.
Kwaupande wake baba wa watoto hao Maulidi Mkuki alipohojiwa, amesema anashangaa kuona mke wake amejifungua mtoto wa aina hiyo wakati yeye ana watoto wengine watatu ambao wamezaliwa bila ya kuwa na matatizo yo yote.
Katika hatua nyingine wagonjwa walio fika kutibiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida mchungaji wa kanisa la Anglikana Harodi Ibuku na mkazi wa Singida Atanas Malya, wamesifu madakta kuendele kutoa huduma.
Wamewashauri kumsikiliza Rais Jakaya Kikwete baada ya kuhutubia Taifa na kuwataka kusitisha mgomo na kuendelea kutoa huduma ili kuokoa maisha ya wagonjwa.