
LICHA ya kuwa na kichanga, staa wa filamu za Kibongo, Flora Festus Mvungi amenaswa usiku wa manane ‘akila bata’ jambo lililozua mshangao kwa wadau waliokuwepo eneo hilo.
Msanii huyo alinaswa na paparazi wetu hivi karibuni ndani ya Ukumbi wa Vijana Social, Kinondoni jijini Dar kulipokuwa na tamasha la vipaji, alipofotolewa picha, aling’aka!.
“Sitaki picha bwana, wewe hujui kama nimetoroka usiku huu kuwa hapa! Naomba ufute hizo picha tafadhali, usiniudhi bwana,” alisema Mvungi huku akikwepa miale ya kamera.