
Nchi ya Tanzania imeingia tena kwenye headline kuhusiana na suala la Madawa ya kulevya baada ya kukamatwa tena kwa Mtanzania mwingine akisafirisha Madawa hayo toka Thailand kuelekea Macao nchini China jumanne iliyopita.
Mtanzania huyo ni msichana ana jumla ya umri wa miaka 28 aitwae Jackie Clief alikamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya Heroin huko Macao nchini China
Dawa hizo zimekutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na wana usalama kisha kufanyiwa X-ray ambapo baada ya kufanyiwa X-ray alikutwa na jumla ya vidonge 66 vikiwa na thamani ya dola za kimarekani 137,72.