
JESHI la polisi jijini Dar limemkamata binti anayefahamika kwa jina la Moza kwa kosa la kudaiwa kumdhalilisha Mtangazaji wa Runinga ya TV1, Ezden Jumanne ambapo anatarajiwa kuburuzwa mahakamani muda wowote baada ya uchunguzi kukamilika.

Moza ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtangazaji huyo kisha kuachwa, anadaiwa kumrekodi video ya utupu Ezden kipindi walipokuwa kwenye uhusiano mzuri kisha kuisambaza mitandaoni walipogombana.
Chanzo makini kimedai kuwa, Moza alikamatwa na kuwekwa mahabusu katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar kufuatia msako mdogo uliofanywa na polisi saa chache baada ya mrembo huyo kuvujisha video hiyo.


“Hakunitendea haki, Nimeshalifikisha suala hili polisi, taratibu za kipolisi zikikamilika anaburuzwa mahakamani,” alisema Edzen.