Meya wa Ilala Jerry Silaa akiongea na Wafanyabiashara wa Soko la wazi lilipo katikati ya Soko Kubwa la Kariakoo na Soko dogo, ni zaidi ya miezi 3 wafanyabiasahara wa soko hilo wamepigwa marufuku kufanya biashara katika eneo hilo.
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa ametembelea kwenye soko la Kariakoo kuongea na wafanyabiashara mbalimbali, kufuatia malalamiko ya kuhamishwa katika soko la wazi na kusababisha wafanyabiashara hao kutangatanga.
Akizungumza na wafanyabiashara hao Meya Silaa alisema kuwa amesikia tatizo la wafanyabiashara hao na anakwenda kuongea na viongozi wa Manispaa hiyo ili kuweza kuandaa utaratibu wa kuwarudisha katika eneo hilo au kuwapeleka sehemu nyingine.